Msanii- Basaga ft Neyba
Wimbo- Kesho Yangu
Producer- Ecko Scott
MP4 JAZZBAND
Intro-Neyba
Naiona keshooooooo.....
Shida changamotoooo....
Verse 01.
Wasiojuwa wanajuwa hii Game tumeanzia hapa/
Kumbe kitambo ni zaidi ya Paka Rapa/
Nipe Hi! nikupe Hi! anhaa tusiishie hapa/
Lengo tufike Mbali na tu'make hizo Chapaa/
Nawashoot wasaliti walioko nami/
Yupi anayenipenda na yupi ananitamani?/
Kwenye Game naona mengi mengine nasema noo/
Mrisho Mpoto kanidhurumu kolabo na Ben Pol/
Ahadi nyingi kaka utakuza Kipaji/
Ujanja mwingi mbele Giza mpenzi mtazamaji/
Wakadiriki kukizima hiki kipaji/
Mpaji ni Mwenyezi aliyejuu/
Waswahili wakasema hii Dunia haiko sawa/
Mtaani Guest nyingi kuliko Duka za Dawa/
Hawa Binadamu Hawa...Ubinadamu kazi/.
kiitikio...Neyba
Naiona keshoo,nitafika mbali iwe kwa shari ama shwarii.....(japo mengi nayapitia)...
Shida changamotoo,zimenifunza mengi nilipotoka ni mbaali ...(mapito ya dunia)..×2
Verse 02.
Nabust future najituma maisha yamegeuka Drama/
Mbele ni giza nene na unene umezidi nyuma/
Nafanya mishe zangu,wanga wanabana/
Nawaumbua nazidi kupambana/
Shukrani kwa Mwenyezi pumzi silipii/
Nikibuma Plan A najiseti Plan B/
Imani tele kama muumini mbele ya Zaka/
Waumini tupo wengi we unashindwa hata Sadaka/
Mapito nayapitia Majonzi ni Moyoni/
Binadamu wengi wao visirani/
Wanatakatisha sura,Mioyoni bado Jiki/
Vikwazo vingi kwenye Kusaka riziki/
Kupata na kufeli yote nashukuru/
Naamini kesho na mimi ntapata Nuru/
Haa haa teh na Famy Two..Baba Raizor..
Kiitikio
Naiona keshoo...nitafika mbali nlipotoka ni mbaali....(japo mengi nayapitiaa)
Shida,Changamotooo zimenifunza mengi nlipotoka ni mbaali....(Mapito ya duniaa)..×2
Kesho nitafika tuuu.......
Outro.
Naioooona Keshooo.......
Ooooooh Yeeea Kesho nitafika tu.
Mp4 Jazzband na King wa Rj
Mchezo umekwishaaaaaa
Source ;
Written by Basaga