Wabunge wa Catalonia wachagua spika kutoka upande wa kujitenga

Wabunge wa jimbo la Catalonia jana wamemchagua mwanasiasa anayeunga mkono kujitenga na Uhispania kama spika wa bunge, ikiwa ni hatua ya kwanza ya mpango wao wa kutaka kumrejesha Carles Puigdemont, kiongozi aliyeondolewa madarakani na ambaye yupo uhamishoni nchini Ubelgiji. Ikiwa ni mara ya kwanza wabunge hao wanakutana tokea jaribio la kutaka kujitenga na serikali kuu ya Uhispania, waandamanaji wanaounga mkono kujitenga wamekusanyika nje ya bunge mjini Barcelona, ambalo lina wingi wa wajumbe wa vyama vinavyounga mkono uhuru wa jimbo hilo baada ya kushinda katika uchaguzi wa jimbo wa Desemba 21.
   Licha ya kuwepo uhamishoni nchini Ubelgiji, Puigdemont anataka kurudi nchini Uhispania na kuliongoza jimbo hilo lililogawanyika. Serikali kuu ya Waziri Mkuu Mariano Rajoy imeonya itakamata udhibiti wa moja kwa moja wa jimbo la Catalonia iwapo Puigdemont atajaribu kuongoza wakati akiwa Ubelgiji, jambo linaloweza kuzua mgogoro mwengine wa kisiasa.


SHARE THIS
Previous Post
Next Post