RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino amewasili nchini leo alfajiri Feb. 22, 2018 kwa ajili ya mkutano wa FIFA unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Infantino akiongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Ahmad Ahmad wali pokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe walioongozana na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Rashid Ali Juma na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar.
Rais huyo wa FIFA akiwa uwanjani hapo baada ya kuwasili alipata fursa ya kuzungumza na waziri M wakyembe ambapo alimtaja nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, anayecheza soka la kulipwa KRC Genk ya Ubelgiji .
Mbwana Samatta akiitumikia Genk.
“Nilisikia mchezaji bora wa Afrika kutoka Tanzania, Mbwana Samatt, anayecheza Genk, hii ni nchi ya mpira licha ya changamoto za shirikisho siku za nyuma, lakini kwa sasa mpo kwenye mstari kutokana na uongozi mpya kwa kushirikiana na CAF na FIFA,” alisema Infantino.
Author: Mdigital beatz
Related Posts
Some simillar article from this label, you might also like
- Blog Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)