Arsenal iliicharaza Crystal Palace
4-1 huku Chelsea ikiifunga mdomo Brighton 4-0 katika mechi za ligi ya
Uingereza siku ya Jumamosi.
The Gunners walikosa huduma za
mchezaji Alexis Sanchez, ambaye anatarajiwa kujiunga na Manchester
United, lakini walikuwa wakiongoza kwa bao 4-0 baada ya dakika 22.Manchester United ambao wako katika nafasi ya pili walipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya wenyeji Burnley, kufuatia bao la Anthony Martial na hivyobasi kupanda wakiwa pointi sita nyuma ya viongozi Manchester City, ambao wanakabiliana na Newcastle katika mechi ya mwisho (17:30 GMT).
Mkufunzi mpya wa Stoke Paul Lambert alianza vizuri , baada ya kuiongoza City kuondoka katika eneo la kushushwa daraja kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Huddersfield, kufuatia mabao ya Joe Allen na Mame Biram Diouf.
Penalti ya Jamie Vardy na bao la Riyad Mahrez lilisaidia Leicester City kuendeleza msururu wa matokeo mabaya wa Watford
Nayo West Ham ilitoka sare ya 1-1 na Bournemouth, baada ya bao la Ryan Fraser la dakika ya 71 kusawazishwa sekunde 69 baadaye na Javier Hernandez.