Jibu la Don Cheadle kuhusu kuigiza kama Robert Mugabe kwenye filamu ya MUGABE.

Mwigizaji mkubwa wa filamu kutoka Marekani
Donald Frank Cheadle Jr aliyeigiza kama Paul Rusesabagina kwenye filamu maarufu ya Hotel Rwanda amepiga chini mchongo wa kuigiza kama Rais Mstaafu Robert Mugabe wa Zimbabwe.
Donald Frank Cheadle Jr alipewa ofa ya kuigiza kama Rais huyo kwenye filamu ya “Mugabe” iliyotakiwa kutoka mwaka 2019, Donald anasema “Africa ilinipigia simu kuhusu kuigiza kama Mugabe, aliyekuwa rais wa Zimbabwe, walitaka niigize kama mtu wa Africa na sio African American, Nikasema hapana, ipite tu”.
Muongozaji wa Filamu hii anatajwa kuwa Director Njagu , aliyetayarisha filamu ya Lobola , kwenye interview alisema “Nampenda Donald ila tumechoka kuwa na wageni wanaoigiza kana watu wetu, tuna waigizaji bora hapa nyumbani, pesa zinaenda Hollywood nasio hapa,tumechoka wao kuja kutumia lafudhi feki za Africa, nimeanza kuifanyia kazi hii filamu, ntatoa taarifa soon”


SHARE THIS
Previous Post
Next Post