Chelsea sasa kukutana na Barcelona au PSG mtoano baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 London dhidi ya Atletico Madrid
Chelsea wameikosa fursa ya kukaa kileleni mwa Kundi C baada ya mechi yao dhidi ya Atletico kuishia sare ya 1-1 Jumanne usiku Ligi ya Mabingwa katika uwanja wa Old Trafford.
Roma ikiipiga Qarabag, Chelsea ilipambana kupata ushindi mjini London lakini waliambulia sare baada ya Stefan Savic kujifunga na kusawazisha goli la Saul Niguez na hakuna timu iliyofanikiwa kuziona nyavu dakika za mwisho.
Wakati Atletico wakishuka Ligi ya Europa, Chelsea watakabiliana na aidha Barcelona au Paris Saint-Germain katika hatua ya 16-Bora za michuano hii baada ya Krismasi.
Atletico walianza kwa nguvu na baada ya muda kidogo wa kumiliki mpira mwanzoni mwamchezo, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Fernando Torres alifanikiwa kupiga shuti kuelekea langoni lakini beki aliokoa na mpira ukapaa juu ya besela.
Chelsea walihitaji dakika 17 walikaribia kupata goli na lilikuwa jaribio zuri ndani ya dakika 45 za mwanzo baada ya Alvaro Morata kupiga shuti nje ya goli umbali wa yadi 20.
CHELSEA (3-4-2-1): Courtois; Azpilicueta, Christensen, Cahill; Moses, Kante, Bakayoko (Pedro 64'), Zappacosta (Willian 73'); Fabregas, Hazard; Morata (Batshuayi 81')
ATLETICO MADRID (4-5-1): Oblak; Gimenez (Vietto 79'), Savic, Lucas, Filipe Luis; Thomas, Gabi (Correa 79'), Koke, Saul, Griezmann; Torres (Carrasco 57')
Author: Mdigital beatz
Related Posts
Some simillar article from this label, you might also like
- Blog Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)