Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido ameshinda tuzo ya MTV EMA 2017 kwenye kipengele cha ‘Best African Act’ ambacho kilikuwa kinawaniwa na wasanii sita kutoka Afrika akiwemo hasimu wake Wizkid.
Wasanii wengine waliokuwepo kwenye kipengele hicho ni NastyC na Babes Wodumo kutoka Afrika Kusini, Nyansiski kutoka Kenya na C4 Pedro kutoka Angola.
Soma zaidi –
Mwaka jana tuzo hiyo ilichukuliwa na Ali Kiba kutoka Tanzania na sherehe za ugawaji wa tuzo hizo mwaka huu zinafanyika leo Novemba 12, 2017 jijini London, nchini Uingereza.