Na oscarnickson19
Majina matano ya wanasoka wanaowania tuzo ya BBC ya mchezaji bora barani Afrika yametajwa ambapo wachezaji kutoka Ligi kuu England wameendelea kumiliki orodha hiyo tangu tuzo hizo zianze kutangazwa. Ambapo klabu ya Liverpool imetoa wachezaji wawili mwaka huu Sadio Mane na Mohamed Salah.
Majina ya wachezaji hao watano ni Pierre-Emerick Aubameyang, Naby Keita, Sadio Mane, Victor Moses na Mohamed Salah.
Jopo la wataalamu na wakongwe wa soka ambalo liliundwa na Emmanuel Amuneke, mshindi wa ubingwa Afrika na Olimpiki 1996, Arnaud Djoum, mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 akiwa na Cameroon, na Jean Sseninde, kutoka Uganda anayechezea Crystal Palace Ladies, walikuwepo kujadili majina ya wachezaji walioteuliwa kushindania tuzo hiyo.
Hata hivyo mshindi wa tuzo hiyo wa mwaka jana, Riyad Mahrez anayekipiga kunako klabu ya Leicester City na timu ya taifa ya Algeria hajatajwa mwaka huu.
1-Naby Keita – RB Leipzig na Guinea
Naby Keita amekuwa gumzo nchini Ujerumani kutokana na kiwango alichokionesha akiwa na klabu ya Rb Leizpg na msimu huu alitajwa katika kikosi bora cha Bundesliga.
Klabu ya Red Bull Leipzig iliwashangaza watu wengi katika msimu wa 2016-17, huku ikimaliza katika nafasi ya pili (na kufuzu katika mashindano ya vilabu bingwa), lakini ilikuwa kiungo huyo wa kati aliyeisadia timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili.
Kwa jumla, alifunga mabao manane, mojawapo likiwa bao lililoorodheshwa kuwania tuzo ya bao bora la msimu huku akitoa usaidizi katika ufungaji wa mabao 7.
2-Pierre-Emerick Aubameyang –Gabon na Borussia Dortmund
Msimu uliopita alifanya makubwa Ujerumani akifunga mabao 35 na kuweka rekodi kuwa mchezaji wa 4 kuwahi kufunga mabao 30 nchini Ujerumani huku akiwa Muafrika wa kwanza kufikisha mabao hayo katika Bundesliga.
3-Sadio Mane –Senegal & Liverpool
Alikuwepo katika kikosi cha Epl cha waandishi wa habari za michezo, alichaguliwa mchezaji bora wa klabu ya Liverpool msimu uliopita huku pia hapo jana akiisaidia Senegal kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa kuichapa Afrika Kusini.
4-Mohamed Salah –Egypt & Liverpool
Ameiwezesha Misri kushiriki michuano ya kombe la dunia lakini msimu uliopita alikuwa na kiwango kizuri sana alipokuwa Fiorentina huku msimu huu akiwa amefunga mabao 7 katika ligi ya Epl.
Victor Moses –Nigeria na Chelsea
Kama ilivyo kwa Salah na Mane huyu naye tayari timu yake imefuzu kuelekea Urusi, Victor Moses tangu kocha Antonio Conte ajiunge na Chelsea amekuwa akimpa sana nafasi japokuwa msimu huu ameandamwa na majeraha yanayomuweka nje hadi sasa.
Author: Mdigital beatz
Related Posts
Some simillar article from this label, you might also like
- Blog Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)