EVERTON KUMCHUKUWA MSHAMBULIAJI WA BESIKTAS CENKTOSUN KWA £27m
Everton wamekubaliana na klabu ya Besiktas ya Uturuki kuhusu kumnunua mshambuliaji Cenk Tosun.
Meneja wa Everton Sam Allardyce amesema kilichosalia sasa ni makubaliano kati ya klabu na mchezaji huyo.
Everton walifanya mkutano na rais wa Besiktas Fikret Orman Jumatano kuhusu uhamisho ambao unatarajiwa kuwa wa £27m.
Tosun, 26, amekuwa London akisubiri idhini ya kukamilisha uhamisho huo.
Allardyce amesema anatumai Tosun atasajiliwa kwa wakati kumuwezesha kucheza dhidi ya Liverpool katika raundi ya tatu ya Kombe la FA Ijumaa.
Tosun aliwasaidia Besiktas kufika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, ambapo watakutana na Bayern Munich.
Allardyce anatarajia mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uturuki ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani atazalisha magoli Everton baada ya klabu hiyo kukaukiwa na mabao baada ya Romelu Lukaku kuhamia Manchester United kwa £90m.
Tosun ndiye mchezaji wa kwanza kununuliwa na Allardyce tangu kuondoka kwa Ronald Koeman.
KOREA KASIKAZINI YAKUBALI MAZUNGUMZO KUHUSU OLIMPIKI
Korea Kaskazini imekubali kushiriki mazungumzo ya ngazi ya juu wiki ijayo kuhusu kushiriki kwa wachezaji wake katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, Korea Kusini imesema.
Mkutano huo wa Januari 9 utaangazia kutafuta njia ya wachezaji wa Korea Kaskazini kushiriki michezo hiyo itakayoandaliwa Korea Kusini Februari.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisema wiki hii kwamba atawatuma wawakilishi katika michezo hiyo na kusema hiyo itakuwa "fursa nzuri ya kuonyesha umoja" miongoni mwa raia wa Korea Kaskazini.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Panmunjom, mpakani.
Eneo hilo linalofahamika kama kijiji cha amani linapatikana katika eneo lisiloruhusiwa kuwa na wanajeshi mpakani, na ni hapo ambapo mazungumzo kati ya nchi hizo yamekuwa yakifanyika tangu zamani.
Kwa mujibu wa afisa kutoka afisi ya rais wa Korea Kusini, mkutano huo utaangazia zaidi michezo hiyo itakayofanyika Pyeongchang.
Hata hivyo, aliambia shirika la habari la Yonhap la Korea Kusini kwamba anaamini kutakuwepo pia na "mazungumzo kuhusiana na kuboresha uhusiano kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini baada ya kuthibitishwa kwa ushiriki wa Kaskazini katika michezo hiyo."
Hayo yatakuwa mazungumzo ya kwanza ya ngazi ya juu kufanyika kati ya nchi hizo mbili tangu Desemba 2015.
Haijabainika ni nani watashiriki mazungumzo hayo.
Korea Kusini yataka mazungumzo na Korea Kaskazini kuhusu michezo
Urusi yafungiwa kushiriki michuano ya olimpiki
Trump: Kibonyezo changu cha nyuklia kina nguvu kuliko cha Kim
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in alikuwa awali amesema anatazama michezo hiyo kama fursa mwafaka ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Mapema wiki hii, Korea Kaskazini ilirejesha mawasiliano ya simu maalum kati ya nchi hizo mbili, kufanikisha mazungumzo hayo.
Hata hivyo, afisa wa wizara ya Korea Kusini kuhusu kuunganishwa kwa mataifa hayo mawili alisema Korea Kaskazini ilikubali mwaliko wa kushiriki mazungumzo hayo kupitia kipepesi.
WAZIRI MWAKYEMBE AJA NA MU ALOVERA NGUMI ZA KULIPWA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) jana tarehe 3 Januari, 2018 amekutana na wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini. Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya Mhe. Waziri na Wadau hao ili kutatua migogoro iliyodumu kwa muda mrefu katika mchezo huo wa masumbwi ya kulipwa, vikao hivyo vilianza mwishoni mwa mwaka 2017.
TAARIFA KWA UMMA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) leo tarehe 3 Januari, 2018 amekutana na wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini. Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya Mhe. Waziri na Wadau hao ili kutatua migogoro iliyodumu kwa muda mrefu katika mchezo huo wa masumbwi ya kulipwa, vikao hivyo vilianza mwishoni mwa mwaka 2017. Katika kikao kilichofanyika leo, Mhe. Waziri aliwaagiza wadau hao kufanya kazi kwa pamoja katika kuunda mfumo mpya utakaolinda maslahi ya mabondia na wahusika wengine wa mchezo wa ngumi za kulipwa na kuliletea Taifa letu heshima kwa kupitia mchezo huo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Ili kupiga hatua, Waziri Mwakyembe ameunda kamati ya watu kumi na moja (11) itakayokusanya maoni ya wadau na kupitia upya katiba ya kuunda Chombo kitakachosimamia mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini. Kamati hiyo imeanza kufanya kazi leo tarehe 03 Januari, 2018 na itakamilisha kazi yake tarehe 31 Januari, 2018. Kamati itasimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na itakuwa na wajumbe wafuatao:-:
1. Ndg. Emmanueli Salehe – Mwenyekiti
2. Ndg. Joe Enea – Makamu Mwenyekiti
3. Ndg. Yahya Pori – Katibu
4. Ndg. Habibu A. Nyogoli – Mjumbe
5. Ndg. Shomari Kimbau – Mjumbe
6. Ndg. Fike Wilson – Mjumbe
7. Ndg. Anthony Ruta – Mjumbe
8. Dkt. Killaga M.Killaga – Mjumbe
9. Ndg. Ally B. Champion – Mjumbe
10. Ndg. Rashidi Matumla – Mjumbe
11. Ndg. Karama Nyilawila – Mjumbe
Aidha, Waziri Mwakyembe ameeleza kwamba katika kipindi cha mpito shughuli za kutoa vibali kwa mapambano ya ndani na kwa mabondia wanaosafiri nje ya nchi zitaendelea kutekelezwa na BMT. “BMT endeleeni kusimamia vibali vya mapambano ya ndani na vibali vya safari za nje ya nchi za mabondia kwa kuzingatia uzalendo, weledi, kanuni na sheria za nchi bila kumwangalia mtu usoni wala kumuonea aya”, amesisitiza Waziri Mwakyembe.
Imetolewa na
Octavian F. Kimario
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
03/01/2018

MAMBO MAKUBWA 13 KATIKA SOKA MWAKA 2017
MWANDEZIMEDIA inakuletea matukio ya soka hapa nchini ambayo hayata sahulika kwa mwaka 2017
1. Ziara ya klabu ya Everton hapa nchini
Moja ya tukio la kukumbukwa kwa 2017 ni ujio wa klabu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza, ziara hiyo ilijumuisha nyota wa kiwango cha dunia kama Wayne Rooney, Jagielka, Ashley William, Lenon, Morgan na wengineyo. Katika ujio huo walifanikiwa kucheza mechi moja dhidi ya Gor Mahia ya nchini Kenya.
2. Serengeti Boys kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17
Kwa mara ya kwanza timu ya Taifa ya vijana inafuzu kushiriki michuano mikubwa barani Afrika baada ya kuwaengua timu ya Congo, licha ya kutofanya vizuri ila ni tukio ambalo litakumbukwa sana kwa mwaka 2017
3.Yanga kutetea taji lake la 3 mfululizo
Mwaka 2017, Yanga waliweka historia baada ya kufanikiwa kunyakua taji la Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo kufuatia kulingana pointi na mtani wake klabu ya Simba ila tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ndiyo sababu ya Wana jangwani hao kuwa mabingwa
4.Simba kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Afrika baada ya takribani miaka 5
Mwaka 2017 ni wa neema kwa klabu ya Simba kwani moja ya tukio watakalo likumbuka ni ubingwa wa kombe la FA walichukua baada ya kumfunga Mbao, na ubingwa huo ukawapa tiketi ya kushirikik kombe la shirikisho Afrika nafasi ywaliyoikosa kwa takribani miaka 5
5.Mchakato wa Mabadiliko katika klabu za Simba na Yanga
Ni moja ya habari iliyosisimua kwa mwaka 2017, ishu ya mabadiliko katika klabu za Simba na Yanga ndiyo ishu kubwa kwa mwaka 2017, kutoka kwenye mfumo wa kizamani wa wanachama hadi kwenda kwenye mfumo wa Hisa
6. Viongozi wa mpira kukamatwa
Tukio lingine kubwa ni kukamatwa kwa viongozi wa mpira wakishitakiwa kwa rushwa na matumamizi mabovu ya Fedha, viongozi hao ni Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu (TFF), Jamal Malinzi na katibu wake Selestini Mwesigwa kadhalika na viongozi wa Simba, Raisi Evans Aveva pamoja na Godfrey Nyange
7. Usajili wa dirisha kubwa kuelekea msimu wa 2017/2018
Tukio lingine lililosisimua ni kipindi cha usajili mkubwa kabla ya msimu wa 2017/2018 kuanza, kikubwa kilicho vutia ni kutokana na majina makubwa kupishana timu, nyota kama Ajibu na Niyonzima sajili zao zilizungumzwa sana kwa mwaka 2017, pia klabu ya Azam kuachana na wachezaji wao walidumu kwa miaka mingi kama Bocco, Manula na Nyoni kadhalika na klabu mpya ya Singida United kushindana na klabu kubwa kwenye kumwaga pesa kwenye kipindi cha usajili
8. Uchanguzi mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF)
Ni tukio kubwa kwa 2017 sababu limefanikisha kupatikana kwa Raisi mpya ambaye ni Wallace Karia ambaye anachukua nafasi ya mtangulizi wake Jamal Malinzi
9. Zanzibar kutinga fainali ya CECAFA
Baada ya kusubili kwa muda mrefu hatimaye mwaka 2017 umekuwa wa neema kwa Zanzibar Heroes baada ya kufanikiwa kutinga fainali ya CECAFA ambayo walipoteza kwa penati dhidi ya wenyeji timu ya Taifa ya Kenya, licha wa mamia kuwadharau ila WaZanzibar waliwashangaza wengi kwa soka safi katika mashindano hayo
10.Simba kuvuliwa ubingwa na timu ya daraja la pili
Ni moja ya tukio lililoacha watu midomo wazi ni kushuhudia klabu ya Simba iliyofanya usajili wa bilioni moja ikivuliwa ubingwa na klabu ya Green Warrior ya daraja la pili
11. Nyota wa Tanzania kupata ulaji nje ya nchini
2017 ni mwaka wa neema kwa Taifa letu baada ya kushuhudia nyota kadhaa wakipata nafasi ya kucheza nje, Simon Msuva amejiunga na Difaa ek Jadida ya Morocco, Abdi Banda yupo Baroka ya Afrika Kusini kadhalika na Dida naye yupo Afrika Kusini, Rashid Mandawa yupo Botswana pia wachezaji kadhaa kupata furs ya kwenda majaribio katika klabu za nje kama, Ndemla, Himid Mao, Yohana Mkomola na wengineyo.
12. Kifo cha kocha Joel Bendera
Kifo cha kocha Joel Bendera ni tukio kubwa kwa mwaka 2017 kwani Bendera ndiye kocha pekee aliyeitoa kimasomaso Taifa Stars katika miaka ya 1980 kwa kuipeleka Nigeria katika michuano ya mataifa Afrika ( AFCON) wakati akifundisha soka
13. Victor Wanyama kupewa mtaa hapa nchini
Ni tukio lililovuta hisia za watu wengi baada ya kushuhudia kiungo anayekipiga timu ya TOttenham Hotspurs akipewa heshima ya kukabidhiwa mtaa, licha ya baadae kuleta mjadala mzito hapa nchini, kiungo huyo alipewa heshima hiyo kufuatia kuhudhuria mashindano ya mtaani yanayo kuja kasi hapa nchini maarufu kama Ndondo ambayo ufanyika kila mwaka katika mikoa mbali mbali
Njombe mji kutesti mitambo
@oscarnickson Club ya Njombe Mji hiii Leo watashuka dimbani jioni ya hii Leo kukibiga dhidi ya maji maji ya songea katika uwanja Wa saba saba mkoani Njombe na afisa habari Wa club hiyo solanus Mhagama amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika