MWANDEZIMEDIA inakuletea matukio ya soka hapa nchini ambayo hayata sahulika kwa mwaka 2017
1. Ziara ya klabu ya Everton hapa nchini
Moja ya tukio la kukumbukwa kwa 2017 ni ujio wa klabu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza, ziara hiyo ilijumuisha nyota wa kiwango cha dunia kama Wayne Rooney, Jagielka, Ashley William, Lenon, Morgan na wengineyo. Katika ujio huo walifanikiwa kucheza mechi moja dhidi ya Gor Mahia ya nchini Kenya.
2. Serengeti Boys kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17
Kwa mara ya kwanza timu ya Taifa ya vijana inafuzu kushiriki michuano mikubwa barani Afrika baada ya kuwaengua timu ya Congo, licha ya kutofanya vizuri ila ni tukio ambalo litakumbukwa sana kwa mwaka 2017
3.Yanga kutetea taji lake la 3 mfululizo
Mwaka 2017, Yanga waliweka historia baada ya kufanikiwa kunyakua taji la Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo kufuatia kulingana pointi na mtani wake klabu ya Simba ila tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ndiyo sababu ya Wana jangwani hao kuwa mabingwa
4.Simba kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Afrika baada ya takribani miaka 5
Mwaka 2017 ni wa neema kwa klabu ya Simba kwani moja ya tukio watakalo likumbuka ni ubingwa wa kombe la FA walichukua baada ya kumfunga Mbao, na ubingwa huo ukawapa tiketi ya kushirikik kombe la shirikisho Afrika nafasi ywaliyoikosa kwa takribani miaka 5
5.Mchakato wa Mabadiliko katika klabu za Simba na Yanga
Ni moja ya habari iliyosisimua kwa mwaka 2017, ishu ya mabadiliko katika klabu za Simba na Yanga ndiyo ishu kubwa kwa mwaka 2017, kutoka kwenye mfumo wa kizamani wa wanachama hadi kwenda kwenye mfumo wa Hisa
6. Viongozi wa mpira kukamatwa
Tukio lingine kubwa ni kukamatwa kwa viongozi wa mpira wakishitakiwa kwa rushwa na matumamizi mabovu ya Fedha, viongozi hao ni Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu (TFF), Jamal Malinzi na katibu wake Selestini Mwesigwa kadhalika na viongozi wa Simba, Raisi Evans Aveva pamoja na Godfrey Nyange
7. Usajili wa dirisha kubwa kuelekea msimu wa 2017/2018
Tukio lingine lililosisimua ni kipindi cha usajili mkubwa kabla ya msimu wa 2017/2018 kuanza, kikubwa kilicho vutia ni kutokana na majina makubwa kupishana timu, nyota kama Ajibu na Niyonzima sajili zao zilizungumzwa sana kwa mwaka 2017, pia klabu ya Azam kuachana na wachezaji wao walidumu kwa miaka mingi kama Bocco, Manula na Nyoni kadhalika na klabu mpya ya Singida United kushindana na klabu kubwa kwenye kumwaga pesa kwenye kipindi cha usajili
8. Uchanguzi mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF)
Ni tukio kubwa kwa 2017 sababu limefanikisha kupatikana kwa Raisi mpya ambaye ni Wallace Karia ambaye anachukua nafasi ya mtangulizi wake Jamal Malinzi
9. Zanzibar kutinga fainali ya CECAFA
Baada ya kusubili kwa muda mrefu hatimaye mwaka 2017 umekuwa wa neema kwa Zanzibar Heroes baada ya kufanikiwa kutinga fainali ya CECAFA ambayo walipoteza kwa penati dhidi ya wenyeji timu ya Taifa ya Kenya, licha wa mamia kuwadharau ila WaZanzibar waliwashangaza wengi kwa soka safi katika mashindano hayo
10.Simba kuvuliwa ubingwa na timu ya daraja la pili
Ni moja ya tukio lililoacha watu midomo wazi ni kushuhudia klabu ya Simba iliyofanya usajili wa bilioni moja ikivuliwa ubingwa na klabu ya Green Warrior ya daraja la pili
11. Nyota wa Tanzania kupata ulaji nje ya nchini
2017 ni mwaka wa neema kwa Taifa letu baada ya kushuhudia nyota kadhaa wakipata nafasi ya kucheza nje, Simon Msuva amejiunga na Difaa ek Jadida ya Morocco, Abdi Banda yupo Baroka ya Afrika Kusini kadhalika na Dida naye yupo Afrika Kusini, Rashid Mandawa yupo Botswana pia wachezaji kadhaa kupata furs ya kwenda majaribio katika klabu za nje kama, Ndemla, Himid Mao, Yohana Mkomola na wengineyo.
12. Kifo cha kocha Joel Bendera
Kifo cha kocha Joel Bendera ni tukio kubwa kwa mwaka 2017 kwani Bendera ndiye kocha pekee aliyeitoa kimasomaso Taifa Stars katika miaka ya 1980 kwa kuipeleka Nigeria katika michuano ya mataifa Afrika ( AFCON) wakati akifundisha soka
13. Victor Wanyama kupewa mtaa hapa nchini
Ni tukio lililovuta hisia za watu wengi baada ya kushuhudia kiungo anayekipiga timu ya TOttenham Hotspurs akipewa heshima ya kukabidhiwa mtaa, licha ya baadae kuleta mjadala mzito hapa nchini, kiungo huyo alipewa heshima hiyo kufuatia kuhudhuria mashindano ya mtaani yanayo kuja kasi hapa nchini maarufu kama Ndondo ambayo ufanyika kila mwaka katika mikoa mbali mbali