Waziri mkuu ampa saa 72 Mkurugenzi kueleza alikopeleka milioni 350

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Bw. Frank Bahati amepewa siku 3 aeleze amepeleka wapi zaidi ya sh milioni 350 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali.
Amri hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.
Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumilia kuona fedha inazopeleka katika halmashauri hiyo kwa ajili ya kugharamia miradi na kulipa madai ya watumishi zinatumika kinyume na maelekezo.
Amesema miongoni mwa fedha hizo ni sh. milioni 451.47 za miradi ya miradi ya maendeleo (CDG), ambapo zilizotumika ni sh. milioni 221.9 tu na kuwataka Mkurugenzi na Muweka hazina wa Halmashauri hii Bw. Peter Molel tarehe 21 mwezi huu kwenda Mwanza kueleza walikopeleka fedha hizo.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa fedha zingine ni sh. milioni 50 za ziizotolewa na Serikali kwa ajili ya kulipa madai mbalimbali ya watumishi kama likizo ambapo zililipwa sh. milioni 13 na zingine hazijulikani


SHARE THIS
Previous Post
Next Post