Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar linadaiwa kuvamia na kuzingira Makao Makuu ya (CUF) Zanzibar bila kufahamika sababu hasa ya kushikilia ofisi hizo.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya muda ya uongozi CUF, Julius Mtatiro na kubainisha kuwa huenda kuna mpango wa kutaka kumkabidhi ofisi hiyo Mwenyekiti wa CUF ambaye anatambulika na Msajili wa vyama vya siasa nchini Profesa Lipumba na kudai wao wanaendelea kufuatilia kujua nini kimewapeleka pale polisi.
“Polisi wakiwa na magari kadhaa, wameivamia Makao Makuu ya Chama cha Wananchi CUF Mtendeni, Zanzibar saa 12.10 jioni hii. Inaonekana/inahisiwa wana ajenda mbili; moja ni kuikalia makao makuu hiyo kimabavu ili kesho Jumatatu waikabidhi kwa Bwana yule ili kutekeleza mkakati maalum”Amesema Mtatiro
“Au wana lengo la kuingia kimabavu na kuweka vitu hatari na kisha kuwakamata viongozi wa CUF na kudai walitunza vitu hatari ofisini hapo. Tunafuatilia jambo hili kwa ukaribu “Ameongez Julius Mtatiro
Chama cha CUF kipo katika mgogoro wa kudumu uliopelekea kuundwa kwa kambi mbili za Maalim Seif na ile ya Pro.Ibrahim Lipumba anayetambulika na Msajili wa vyama vya siasa nchini.
Author: Mdigital beatz
Related Posts
Some simillar article from this label, you might also like
- Blog Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)