UMTITI KUIKOSA ELCLASSICO

KLABU ya Barcelona imepata pigo baada ya beki wake, Samuel Umtiti kuumia nyama za paja na atatakiwa kuwa nje hadi mwaka mpya, maana yake ataikosa El Clasico dhidi ya mahasimu, Real Madrid .
Vigogo wa Katalunya walilazimishwa sare ya 2-2 na Celta Vigo Jumamosi Uwanja wa Nou Camp, mabao yao yakifungwa na nyota wake, Lionel Messi na Luis Suarez .
Lakini vinara hao wa La Liga wakamaliza mchezo huo na pigo zaidi baada ya Umtiti kuumia.
Umtiti mwenye umri wa miaka 24, alikuwa anamdhibiti mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Iago Aspas wakati anaumia.
Barcelona imethibitisha Samuel Umtiti atakuwa nje hadi mwakani baada ya kuumia nyama za paja


SHARE THIS
Previous Post
Next Post