Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 18-19.02.2018
Real Madrid wanataka kumuuza kwa zaidi ya pauni milioni 100 kwa wing'a Gareth Bale ili kumununua mashambulizi wa Chelesea Eden Hazard, 27. (Sunday
Chelsea watamuuliza mshambulizi raia wa Argentina Sergio Aguero, 29, ikiwa Manchester City iliongea na Hazard. (Star
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alijibizana na kiungo wa kati mfaransa Paul Pogba na mlinzi raia wa England Phil Jones baada ya kikosi chake kulimwa na Newcastle wiki iliyopita. (Sun on Sunday)
Mourinho alifanya mkutano wa saa moja kukana tofauti zake na Pogba.
Kipa ya Manchester United na Uhispania David de Gea, 27 anasema ana furaha sana klabuni licha ya ripoti kuwa anataka kuhamia Madrid. (Star on Sunday)
Meneja wa Real Zinedine Zidane ambaye amekuwa chini ya shinikizo huko Bernabeu anasema kusimamia mabingwa hao wa uhispania ni kazi ngumu. (Sunday Times - subscription required).
Manchester City wanammezea mate kiungo wa kati wa Dortmund Julian Weigl, 22, lakini klabu hiyo ya Ujerumani inataka pauni milioni 40 kwa mchezaji huyo. (Sunday Mirror)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kumsani mshambuliaji raia wa Brazil Richarlison na kiungo wa kati mfaransa Abdoulaye Doucoure, 25, kutoka watford kwa pauni milioni 50. (Sun on Sunday)
Mzaliwa wa Jamaica wing'a wa Bayer Leverkusen Leon Bailey, 20, yuko sawa kuichezea England kwa kuwa babu na bibi yake wana paspoti za Uingereza. (Sunday Mirror)
Wing'a wa Liverpool Sadio Mane, 25, anaweza kupewa mkataba ulioboreshwa huko Anfield. Raia huyo wa senegal amebaki na miaka mitatu ya mkataba wake wa puani 80,000 kwa wiki. (Sunday Mirror)
Wing'a wa zmania wa Bayern Munich raia wa uholanzi Arjen Robben, 34, anasema hana mipango ya kustaafu na anataka aidha kuhamia Marekani, China au Qatar. (Sportbuzzer - in Dutch)