TETESI ZA SOKA ULAYA LEO TAREHE 8/1/2017

Mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 26, ataitisha pauni 400,000 kwa wiki kuzuia ofa ya Chelsea ili kujiunga na Manchester United. (Sun)

Chelsea wanamtaka mshambuliaji wa Borussia Monchengladbach na Ubelgiji Thorgan Hazard, 24, kujiunga na ndugu zake Eden, 27, na Kylian, 22, huko Stamford Bridge. (Bild - in German)

Coutinho asema kutua Barca ndoto zimetimia
Liverpool wanamtaka mshambuliaji wa Monaco na Ufaransa Thomas Lemar, 22, kuchukua mahala pake Philippe Coutinho - na wanataka kufanya hilo wiki hii. (Mirror)

Real Madrid walikuwa na nia ya kutoa ofa ya paunia milioni 177 kwa Coutinho kabla ya kukubalia kujiunga na Barcelona kwa pauni milioni 142. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Nottingham yaitupa nje ya kombe la Fa Arsenal
Coutinho atafanyiwa uchunguizi wa kiafya leo Jumatatu na kutangazwa rasmi kama mchezaji wa Barcelona lakini kuanza kwake kunaweza kuchelewewashwa kutokana na jeraha.

Liverpool watajaribu kumleta kiungo wa kati wa RB Leiozig na Guinea Naby Keita Anfield na wana nia ya kulipa zaidi kumpata mchezaji huyo wa miaka 22 mwezi Januari. (Telegraph)

Wing'a mbrazil Lucas Moura, 25, anataka kuondoka Paris St-Germain kujiunga na Manchester United mwezi huu. (Telefoot via Express)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anasema klabu yake haiko tayari kuongeza wachezaji zaidi Januari baada ya kumnunua kijana kutoka Ugiriki wa umri wa miaka 20, Konstantinos Mavropanos. (Sun)


SHARE THIS
Previous Post
Next Post