POLEPOLE ATISHIA KUIPIGA BOMU CHADEMA DAR

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole ametishia kung’oa kiongozi wa Chadema ndani ya mkoa wa Dar es salaam.
Polepole ameyasema hayo baada ya madiwani wawili wa CHADEMA kuachia ngazi Mjini Iringa jana, ambapo amesema kuwa wamekihama chama hicho kwa kumuunga mkono Rais Magufuli na hawawezi kumuunga wakiwa nje ya chama.

“Leo Madiwani wengine wawili wamehama na kujiunga na CCM. Ukiwasikiliza kilichowaondoa ni Uongozi Mbovu na Ubabe pale Iringa Mjini. Nasikia wameambiwa “never outshine your master”. Mimi nilidhani “masta” ni wananchi kumbe ni “pasta”. Ukitukana tusi moja Kiongozi mmoja nachomoa DSM ” ameandika Polepole katika ukurasa wake wa Twitter
Siku kadhaa kumekuwepo madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhamia chama tawala cha CCM.


SHARE THIS
Previous Post
Next Post