UFAFANUZI JUU YA WANAFUNZI WANAKATA RUFANI YA MKOPO (LOAN APPEALS)

HIKI NDICHO WALICHO KIANDIKA BODI YA MIKOPO KUPITUA  AKAUNTI YAO YA TWITER ---HESLB (@HESLBTanzania)

#Ufafanuzi Waombaji waliofiwa na wazazi wanapaswa kuthibitisha uyatima wao kwa kuwasilisha vyeti vya vifo vya wazazi wao kutoka RITA.
— HESLB (@HESLBTanzania) November 6, 2017
#Ufafanuzi Waombaji wa mikopo wenye ulemavu wanapaswa kuambatisha barua kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa inayothibitisha ulemavu huo
— HESLB (@HESLBTanzania) November 6, 2017
#Ufafanuzi Waombaji waliofadhiliwa kwenye masomo yao kabla ya chuo kikuu wanawasilisha uthibitisho wa maandishi ufadhili huo.
— HESLB (@HESLBTanzania) November 6, 2017
#Ufafanuzi Moja ya sifa kuu ni lazima kupata udahili (admission) au kuthibitisha udahili katika chuo kimoja na mkopo utapelekwa huko.
— HESLB (@HESLBTanzania) November 6, 2017
#Ufafanuzi Bajeti ya jumla ya mikopo kwa mwaka 2017/2018 ni TZS 427.54 bilioni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 122,623.
— HESLB (@HESLBTanzania) November 6, 2017
#Ufafanuzi Fedha zinazohitajika kwa malipo kwa ajili ya Robo ya 1ya mwaka 2017/2018 ni TZS 147.06 bilioni ambazo tayari Bodi imezishapokea.
— HESLB (@HESLBTanzania) November 6, 2017
#Ufafanuzi Tutaanza kupokea rufaa J3, Nov13,17 ili kuwapa fursa waombaji ambao hawajaridhika kuwasilisha rufaa kupitia vyuo vyao.
— HESLB (@HESLBTanzania) November 6, 2017
#Ufafanuzi Maelezo ya kina kuhusu utaratibu wa rufaa yatatolewa kupitia tovuti ya Bodi ( https://t.co/mxxg3xuZNf ).
— HESLB (@HESLBTanzania) November 6, 2017
#Ufafanuzi Tunatoa wito kwa uongozi wa vyuo vyote kupokea maombi ya rufaa za wanafuzi na kuwasilisha kwa Bodi ya Mikopo.
— HESLB (@HESLBTanzania) November 6, 2017
#Ufafanuzi Lengo ni kutoa orodha ya waombaji waliofanikiwa rufaa zao kabla ya Novemba 30, 2017.
— HESLB (@HESLBTanzania) November 6, 2017
#Ufafanuzi Ikiwa unahitaji ufafanuzi wowote, tuandike info@heslb.go.tz au tuandikie hapa
— HESLB (@HESLBTanzania) November 6,

HESLB

SHARE THIS
Previous Post
Next Post