NANDY : SIKUWAZA KABISA KUHUSU KILICHOTOKEA
Msanii wa bongo fleva Nandy ambae anaonekana ni mwenye njaa na mafanikio kimuziki leo ameamua kuongea ya moyoni kuwa hakuwa na mategemeo kuwa angeweza kubeba tuzo ya Afrima. Nandy ambae alikuwa na hofu mara baada ya kushindanishwa na wasanii ambao wameshamtangulia kufahamika kimataifa kama vile Vanessa Mdee , JulianaKanyomozi na
Victoria Kimani ambao wote walikuwa katika kipengele kimoja cha Best Female Eastern Africa ambapo Nandy aliibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho.
Nady ameyasema hayo mapema leo wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Clouds 360 kupitia CloudsTv . Kikubwa zaidi unaambiwa wakati anatangazwa mshindi katika kipengele hicho Nandy aliamua kuziba masikio ili asisikie nani ndio mshindi lakini cha ajabu jina lake ndio akasikia linatajwa.