BALE PANCHA NYINGIiiiiiii

Na oscarnickson19. Tokea amejiunga na Real Madrid Juni, 2013 kiungo Gareth Bale, ameumia na kulazimika kukaa nje ya uwanja mara 24.
Alianza kwa kuumia nyama, baadaye ikafuatia enka na akalazimika kufanyiwa upasuaji.
Kutokana na kuandamwa na majeraha mara kwa mara alishindwa kucheza mechi 17 mfululizo katika msimu wa 2016/17.
Kabla ya hapo katika msimu wa In 2015/16, Bale alikosa mechi 19 katakana na tatizo la nyama au misuli.
Msimu wa 2013/14, akiwa mbichi kabisa alikosa mechi 15 kutokana na tatizo hilo la misuli.
Kama utazungumzia mechi za mashindano ambazo amekosa tokea amejiunga na Real Madrid akitokea Tottenham ya England, ni 79.


SHARE THIS
Previous Post
Next Post