HARRY KANE: "SARE DHIDI YA MADRID NI ISHARA KUWA SPURS INAENDELEA"

Tottenham waliondoka Santiago Bernabeu wakiwa na pointi moja baada ya kuwang'ang'ania mabingwa hao kwa sare ya 1-1 Jumanne
Harry Kane amedai kuwa sare ya Jumanne usiku ya 1-1 dhidi ya Real Madrid kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa imeonyesha ni jinsi gani Tottenham Hotspur wamekuwa timu.
Kikosi cha Mauricio Pochettino kilipata goli la kuongoza dakika ya 28 katika uwanja wa Bernabeu baada ya Raphael Varane kujifunga akigongana na krosi ya Aurier.
Los Blancos walisawazisha kabla ya muda wa mapumziko, hata hivyo, baada ya Aurier kumchezea rafu Toni Kroos adhabu ya tuta ilitolewa, Cristiano Ronaldo bila kufanya makosa alifunga kutokea yadi 12.
"Tumefurahi. Walipata nafasi lakini tulicheza na tuliyafanya maisha yao kuwa magumu," Kane aliliambia BT Sport.
"Pointi moja Bernabeu, ni kama pointi moja kila siku ya wiki. Inaonyesha kuwa timu yetu inapevuka."
"Imetuweka kwenye nafasi nzuri na tutacheza nao tena mechi ya marudiano. Hii imeonyesha kuwa kucheza katika kiwango kikubwa kama hiki."
Matokeo hayo yameipandisha Tottenham juu ya Real Madrid kwenye kundi H ikiwa ni nusu ya safari ya hatua ya makundi, baada ya kufunga magoli mengi ya ugenini kuliko wapinzani wao.


SHARE THIS
Previous Post
Next Post